BREAKING NEWS: Download all selected form six student to join military service JKT 2019 - MWANAHARAKATI BLOG

MWANAHARAKATI BLOG

Blog About Academics, Notes, Syllabus, Jobs, Music, sports and games

Search Here

Post Top Ad

Wednesday 22 May 2019

BREAKING NEWS: Download all selected form six student to join military service JKT 2019

BREAKING NEWS:FORM SIX WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JKT (Kwa mujibu wa sheria 2019)



TAARIFA KWA UMMA
WITO WA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT MUJIBU WA SHERIA MWAKA 2019


Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), limechagua vijana waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita kwa mwaka 2019, kutoka shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa Sheria.
Sanjari na uchaguzi huo, JKT limewapangia makambi watakayokwenda kupatiwa mafunzo kwa muda wa miezi mitatu na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 01 hadi 07 Juni 2019.
Vijana waliochaguliwa wamepangiwa katika kambi za JKT Rwamkoma-Mara, JKT Msange-Tabora, JKT Ruvu-Pwani, JKT Mpwapwa na JKT Makutupora-Dodoma, JKT Mafinga-Iringa, JKT Mlale-Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba-Tanga, JKT Makuyuni-Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa, na JKT Mtabila –Kigoma, JKT Itaka-Songwe, JKT Lua na JKT Milundikwa-Rukwa, JKT Nachingwea-Lindi.
Aidha, wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (physical disabilities) wanatakiwa kuripoti kambi ya JKT Ruvu iliyopo Mlandizi mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo.
JKT linawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa vifuatavyo:-
  1. Bukta ya rangi ya ‘Dark Blue’ yenye mpira kiunoni (lastic), iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini, isiyo na zipu.
  2. Raba za michezo zenye rangi kijani au blue.
  3. Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari.
  4. Soksi ndefu za rangi nyeusi.
  5. Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi.
  6. Track suit ya rangi ya kijani au blue
  7. Nauli ya kwenda makambini na kurudi nyumbani.
Mkuu wa JKT anawakaribisha vijana wote waliochaguliwa ili waweze kujiunga na vijana wenzao katika kujifunza uzalendo, umoja wa kitaifa, stadi za kazi, stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa letu.
Kuona orodha kamili ya majina ya vijana waliochaguliwa na maeneo ya makambi ya JKT waliyopangiwa bofya kwenye jina la kambi hapo chini

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano,
Makao Makuu ya JKT,
Tarehe 22 Mei 2019.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages