WhatsApp yasaidia ndugu kutambua maiti wao - MWANAHARAKATI BLOG

MWANAHARAKATI BLOG

Blog About Academics, Notes, Syllabus, Jobs, Music, sports and games

Search Here

Post Top Ad

Thursday 9 March 2017

WhatsApp yasaidia ndugu kutambua maiti wao


Maiti huyo ambaye alibaki hospitalini hapo kwa saa 12, juzi ndugu zake walithibitisha kwamba alikuwa ni ndugu yao baada ya picha iliyopigwa na kutumwa kwenye mtandao wa WhatsApp kusaidia kutambuliwa.
Ndugu hao waliichukua maiti hiyo juzi saa 2:00 usiku na kwenda kuizika eneo la Marangu Samanga.
Akizungumza na mwandishi wetu jana, Roman Mongi, ambaye ni ndugu wa marehemu Frank Mongi, alisema awali waliukataa mwili huo kwa kuwa ndugu yao alikuwa mwembamba lakini maiti ilionyesha alikuwa mnene.
Alisema walipokuta maiti imewekewa lebo yenye jina la Ibrahim Msuya, waliwasiliana na ndugu wa marehemu huyo waliokuwa wilayani Mwanga.
“Walitutaka tuupige picha huo mwili uliokuwa na jina la Ibrahim Msuya, halafu tuwatumie picha kwa WhatsApp. Ndipo wakasema hakuwa ndugu yao na kwamba waliouchukua ndiyo wa kwao,” alisema.
By:jux mkinga
Chanzo: Mwananchi

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages